Na Mwandishi Wetu
Sasa ni dhahiri kwamba Tanzania itakuwa na Makamu wa Rais mpya baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuridhia kujiuzulu kwa Dkt Emmanuel Nchimbi aliyekuwa akishikilia wadhifa huo.
Dkt Nchimbi alijiuzulu nafasi hiyo jana Jumanne Agosti 25, 2026 katika barua aliyomwandikia Rais Samia akisema kuwa amejiridhisha pasipo shaka kuwa Rais anatamani mabadiliko na yeye (Nchimbi) yuko tayari kuachia nafasi hiyo kwa mtu mwingine.
Taarifa fupi yenye aya mbili iliyotolewa na Ikulu jana na kusainiwa na Katibu Mkuu Kiongozi, Dkt Moses Kusiluka, ilisema kuwa Rais Samia ameridhia ombi la kujiuzulu kwa Dkt Nchimbi.
Barua hiyo iIieleza kuwa taratibu za kikatiba za kumpata Makamu wa Rais
mwingine wa Jamhuri ya Muungano zinachukuliwa.
Dkt Nchimbi atakoma kuwa Makamu wa Rais Septemba 4, 2026, kwa mujibu wa barua aliyomwandikia Rais kuhusu kujiuzulu kwake.
Katiba ya sasa ya Tanzania ya mwaka 1977 inaeleza waziwazi kwamba uteuzi wa Makamu wa Rais ni lazima uthibitishwe na Bunge la Jamhuri ya Muungano baada ya kupendekezwa na mamlaka ya uteuzi.
![]() |
| Dr Emmanuel Nchimbi |
Watanzania wa kila rika na kila tabaka la jamii wanasubiri kwa hamu kuona jinsi taifa linavyojinyumbua katika kuketa mabadiliko ya uongozi wa juu, hasa uteuzi wa Makamu wa Rais ajaye kuelekea 2030.
Kama walivyo wabashiri wa mambo ya siasa, tayari kuna minong'ono ya kisirisiri ya majina ya watu wanaotajwa kumrithi Dkt Nchimbi.


No comments:
Post a Comment