NEWS

Friday, 6 November 2026

Mahakama yamhukumu Lissu kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani



Tundu Lissu akiwa mahakamani

Mahakama Kuu ya Tanzania, Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, imemhukumu Mwenyekiti wa chama cha upinzani - CHADEMA Taifa, Tundu Lissu, kutumikia kifungo cha miaka minne gerezani, baada ya kumkuta na hatia ya kosa la uchochezi.

Mahakama pia imemesema Lissu ana haki ya kukata rufaa dhidi ya hukumu hiyo.

Uamuzi huo umetolewa leo Ijumaa, Novemba 6, 2026 na kuhitimisha kesi iliyodumu kwa takribani miezi 19 tangu kukamatwa kwake.

Awali, Lissu alishatkiwa kwa kosa la uhaini, lakini leo hakukutwa na hatia ya kosa hilo kupitia kesi ya uhaini namba 000019605 ya mwaka 2025.

Lissu alikamatwa Aprili 9, 2025 mjini Mbinga, mkoani Ruvuma, muda mfupi baada ya kuhutubia mkutano wa CHADEMA uliokuwa sehemu ya kampeni ya chama hicho ya No Reforms, No Election.

Siku iliyofuata alifikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam na kusomewa mashtaka ya uhaini.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages