
Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi (kulia) na Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, wakifurahia jambo kwenye Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania unaofanyika jijini Dar es Salaam kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026.
Dar es Salaam
-------------------
Makamu wa Rais, Deogratius Ndejembi, anamwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa Mkutano wa Saba wa Kimataifa wa Uwekezaji katika Sekta ya Madini Tanzania (TMIC 2026).
Mkutano huo unafanyika kuanzia Novemba 19 hadi 21, 2026 katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere (JNICC) jijini Dar es Salaam.
Wizara ya Madini imeandaa mkutano huo kwa kushirikiana na Chemba ya Migodi Tanzania.
Washiriki ni pamoja na viongozi na wawakiishi kutoka nchi mbalimbali za Afrika, kampuni za madini, wawekezaji, taasisi za fedha na watoa huduma za teknolojia.
Majadiliano yanahusu fursa za uwekezaji katika dhahabu, kinywe, nikeli, shaba, madini adimu na niobiamu, pamoja na namna ya kuongeza ushiriki wa wachimbaji wadogo na kampuni za Kitanzania katika mnyororo wa thamani wa madini.

No comments:
Post a Comment