NEWS

Monday 29 July 2019

MENO YA TEMBO YA MAMILIONI YA FEDHA YAKAMATWA TARIME | + VIDEO\


Na Clonel Mwegendao 

Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa kushirikiana na  kikosi kazi cha taifa cha (task force) wamefanikiwa kukamata meno ya tembo matano ( 5)  yenye thamani ya Shilingi Milioni  170.7 
“ Watuhumiwa walikuwa wameyahifadhi meno hayo kwenye mfuko wa sandarusi na walikuwa wanayasafirisha kwa kutumia pikipiki yenye namba za usajili MCBQB aina ya Sanlg”  Kamanda wa Polisi Tarime Rorya(RPC) Henry Mwaibambe amewambia waandishi wa habari ofisini kwake mjini Tarime leo
Meno hayo yenye uzito wa kilo 24.55 yalikamatwa  Julai 18 mwaka huu katika kijiji cha Ng’ereng'ere Kata ya Regicheri .
“ Askari polisi wakiwa katika msako pamoja na kikosi cha 'task force' taifa walifanikiwa  kuwakamata Mseti  Daniel (27) mkazi wa kijiji cha Nyabitoche  na Peter Moina(25) mkazi wa kijiji cha Nge’ereng’ere wakiwa  na meno ya tembo matano “, RPC Mwaibambe  amesema.


Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani Julai 26 kwa kosa la uhujumu uchumi, amesema RPC Mwaibambe.
Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa wananchi  kuendelea kutoa ushirikiano ambao utasadia kokomesha ujangili ambao unahatarisha uwepo wa  tembo na wanyama wengine ambao  ni rasilimali muhimu kwa taifa.
Wakati huohuo  RPC Mwaibambe amesema Julai 28  katika  maeneo ya Mtana  Kata ya Manga , askari polisi walijibu mashambulizi ya watu wanaodhaniwa  kuwa ni majambazi na katika tukio hilo  mtuhumiwa mmoja Joshua Nyamanche alijeruhiwa na kufariki muda mfupi akiwa njiani  akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
“ Katika eneo la tukio askari wetu walipata Bastola moja ambayo imefutwa namba ikiwa na risasi tatu kwenye magazine na maganda mawili ya risasi za Bastola” amesema Kamanda Mwaibambe.
Aidha Kamanda Mwaibambe amesema watuhumiwa wengine wawili walifanikiwa kukimbia na juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.
RPC Henry Mwaibambe akionesha bastola iliyotumiwa na watu watatu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi kurushiana risasi na askari polisi Julai 28 katika  eneo la Mtana kata Manga Wilayani Tarime( Picha zote na Clonel Mwegendao )

TAZAMA VIDEO HAPA CHINI


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages