Jeshi la Polisi Mkoa wa Polisi Tarime Rorya kwa
kushirikiana na  kikosi kazi cha taifa cha
(task force) wamefanikiwa kukamata meno ya tembo matano ( 5)  yenye thamani ya Shilingi Milioni 
170.7 
“ Watuhumiwa walikuwa wameyahifadhi meno hayo kwenye
mfuko wa sandarusi na walikuwa wanayasafirisha kwa kutumia pikipiki yenye namba
za usajili MCBQB aina ya Sanlg”  Kamanda
wa Polisi Tarime Rorya(RPC) Henry Mwaibambe amewambia waandishi wa habari
ofisini kwake mjini Tarime leo
Meno hayo yenye uzito wa kilo 24.55 yalikamatwa  Julai 18 mwaka huu katika kijiji cha Ng’ereng'ere
Kata ya Regicheri .
“ Askari polisi wakiwa katika msako pamoja na
kikosi cha 'task force' taifa walifanikiwa  kuwakamata Mseti  Daniel (27) mkazi wa kijiji cha
Nyabitoche  na Peter Moina(25) mkazi wa
kijiji cha Nge’ereng’ere wakiwa  na meno
ya tembo matano “, RPC Mwaibambe  amesema.
Watuhumiwa wote walifikishwa mahakamani Julai 26 kwa
kosa la uhujumu uchumi, amesema RPC Mwaibambe.
Kamanda Mwaibambe ametoa wito kwa wananchi  kuendelea kutoa ushirikiano ambao utasadia
kokomesha ujangili ambao unahatarisha uwepo wa  tembo
na wanyama wengine ambao  ni rasilimali
muhimu kwa taifa.
Wakati huohuo 
RPC Mwaibambe amesema Julai 28  katika 
maeneo ya Mtana  Kata ya Manga , askari
polisi walijibu mashambulizi ya watu wanaodhaniwa  kuwa ni majambazi na katika tukio hilo  mtuhumiwa mmoja Joshua Nyamanche alijeruhiwa
na kufariki muda mfupi akiwa njiani  akipelekwa hospitali kwa ajili ya matibabu.
“ Katika eneo la tukio askari wetu walipata Bastola moja ambayo imefutwa namba ikiwa na risasi tatu kwenye magazine na maganda mawili ya risasi za Bastola” amesema Kamanda Mwaibambe.
“ Katika eneo la tukio askari wetu walipata Bastola moja ambayo imefutwa namba ikiwa na risasi tatu kwenye magazine na maganda mawili ya risasi za Bastola” amesema Kamanda Mwaibambe.
Aidha Kamanda Mwaibambe amesema watuhumiwa wengine
wawili walifanikiwa kukimbia na juhudi za kuwatafuta bado zinaendelea.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI


 
 
 
 
 
 
.jpeg) 
No comments:
Post a Comment