NEWS

Thursday 18 July 2019

MWANAHABARI EVA SWEET AFARIKI DUNIA


Na mwandishi wetu, Musoma
Mwanahabari  Eva sweet Msiba  amefarika dunia jana Jumatano katika hospitali  ya Mkoa wa Mara iliyopo mjini Musoma kutokana na tatizo saratani ya titi.
“ Eva alifariki dunia jana majira ya saa moja jioni  na mazishi yake yatafanyika kesho( Ijumaa) hapa Musoma “, Gabriel Kambuga ambaye ni mume wa Eva Sweet amesema katika mazungumzo mafupi na Mara Online News leo asubuhi.
Mbali na kuwa mwanahabari Eva Sweet  alikuwa ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwaka 2015 aligombea nafasi ya ubunge Viti Maalumu kupitia CCM Mkoa wa Mara.
Hadi mauti yanamfika Eva ameacha mume na watoto wawili ambao ni Andrew na Fanuel
    Pumzika kwa amani Eva Sweet !


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages