Na mwandishi wetu, Musoma
Mwanahabari Eva sweet Msiba amefarika dunia jana Jumatano katika hospitali
ya Mkoa wa Mara iliyopo mjini Musoma
kutokana na tatizo saratani ya titi.
“ Eva alifariki dunia jana majira ya saa moja jioni na mazishi yake yatafanyika kesho( Ijumaa)
hapa Musoma “, Gabriel Kambuga ambaye ni mume wa Eva Sweet amesema katika
mazungumzo mafupi na Mara Online News leo asubuhi.
Mbali na kuwa mwanahabari Eva Sweet alikuwa ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na mwaka 2015
aligombea nafasi ya ubunge Viti Maalumu kupitia CCM Mkoa wa Mara.
Hadi mauti yanamfika Eva ameacha mume na watoto
wawili ambao ni Andrew na Fanuel
Pumzika
kwa amani Eva Sweet !
No comments:
Post a Comment