Mbunge wa Bumbuli (CCM) January Makamba |
Na mwandishii wetu
Rais John Magufuli leo Julai 21 ametengua uteuzi wa
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano
na Mazingira) January Makamba na kumteu George
Simbachawene kuchukua nafasi yake.
Taarifa ya Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu,
Gerson Msigwa ambayo imetolea kwa vyombo vya habari leo asubuhi imesema Rais
Mgufuli pia amemteua Hussein Bashe kuwa Naibu Waziri wa Kilimo kuchukua nafasi ya Innocent Bashungwa ambaye
aliteuliwa kuwa Waziri wa Viwanda na Biashara hivi karibuni.
Rais Magufuli pia amemteua Balozi Martin Lumbanga
kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibithi wa Ununuzi wa
Umma(PPRA) kushika nafasi hiyo kwa kipindi cha pili.
“ Uteuzi wa viongozi hao unaanza leo tarehe 21 Julai,2019”, imesema
taarifa hiyo.
“
No comments:
Post a Comment