Na mwandishi wetu
Watu 4 wamefariki dunia na wengine 15 kujeruhiwa katika ajali ambayo imehusisha magari mawili aina ya Toyota Hiace na LandCruiser katika Wilaya ya Kahama Mkoani Shinyanga .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Shinyanga(RPC) Richard
Abwao amesema ajali hiyo ilitokea jana usiku Julai 21 katika eneo la Nyambula
kata ya Ngogwa.
“ Waliokufa ni 4 wakiwemo watoto watatu na mtu mzima
mmoja na majeruhi ni 15 ambao wanapata
matibabu katika hospitali ya Kahama”, RPC Abwao ameiambia Mara Online News kwa
njia ya simu leo asubuhi.
RPC Abwao
amesema hali za majeruhi zinaendelea vizuri.
“ Tunawashikiria pia madereva wote wawili ambao pia
ni majeruhi na wapo hospitali”, aliongeza
No comments:
Post a Comment