Mkuu wa Wilaya ya Tarme Charles Kabeho akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo August 13 kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura (picha na Mara Online News) |
Na Clonel
Mwegendao, Tarime
Zoezi la kuboresha
daftari la wapiga kura limeanza leo August 13 katika majimbo yote mawili ya Wilaya
ya Tarime huku Mkuu wa Wilaya hiyo Charles akitoa onyo kali kwa wale wote wasiokuwa
na sifa kuijiandikisha wasijaribu kufanya hivyo .
“ Tumejipanga vizuri kuhakikisha kila anayejiandikisha
ana sifa , wale ambao hawana sifa wasijipeleke“, Kabeho amewambia waandishi wa habari ofisini
kwake leo mchana.
Aidha DC Kabeho ametoa wito kwa wananchi wote wenye
sifa kujiandikisha baadala ya kusubiri dakika ya mwisho .
Afisa Mwandikishaji
Jimbo la Tarime Mjini Elias Ntiruhungwa amesema zoezi hilo limeanza saaa mbili
asubuhi katika vituo vyote 93 na linaendelea vizuri katika Halmashauri ya Mji
wa Tarime.
Ntiruhungwa
ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime pia ametoa wito kwa vijana wote na kila mwananchi
mwenye sifa kujitokeza kujiandikisha .
“ Zoezi linachukua siku saba, limeanza leo August 13 na tusingependa kuona mwananchi
mwenye sifa anabaki bila kuandikishwa “, amesema Ntirihungwa akikagua zoezi hilo katika kata ya Turwa eneo
la Rebu .
TAZAMA VIDEO:
No comments:
Post a Comment