NEWS

Tuesday 13 August 2019

UBORESHAJI WA DAFTARI LA WAPIGA KURA: DC KABEHO AONYA WASIOKUWA NA SIFA WASIMJARIBU | +VIDEO

Mkuu wa Wilaya ya Tarme Charles Kabeho akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake leo August 13 kuhusu zoezi la uboreshaji wa daftari la wapiga kura (picha na Mara Online News)

Na Clonel  Mwegendao, Tarime
Zoezi la kuboresha  daftari la wapiga kura limeanza leo August 13  katika majimbo yote mawili ya Wilaya ya Tarime huku Mkuu wa Wilaya hiyo Charles akitoa onyo kali kwa wale wote wasiokuwa na sifa kuijiandikisha wasijaribu kufanya hivyo .
“ Tumejipanga vizuri kuhakikisha kila anayejiandikisha ana sifa , wale ambao hawana sifa wasijipeleke“,  Kabeho amewambia waandishi wa habari ofisini kwake leo mchana.
 Aidha   DC Kabeho ametoa wito kwa wananchi wote wenye sifa kujiandikisha baadala ya kusubiri dakika ya mwisho .
Afisa Mwandikishaji  Jimbo la  Tarime Mjini  Elias Ntiruhungwa  amesema zoezi hilo limeanza saaa mbili asubuhi  katika vituo vyote 93 na  linaendelea vizuri katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Ntiruhungwa  ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime pia  ametoa wito kwa vijana wote na kila mwananchi mwenye sifa kujitokeza kujiandikisha .
“ Zoezi linachukua siku saba, limeanza leo  August 13 na tusingependa kuona mwananchi mwenye sifa anabaki bila kuandikishwa “, amesema Ntirihungwa  akikagua zoezi hilo katika kata ya Turwa eneo la Rebu .

TAZAMA VIDEO:

               

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages