Chama cha watu wenye uwalibino kimepanga kuzindua programu maalumu ambayo inalenga kukuza kipato cha watu wenye ualibino na utalii wa ndani.
 Uzinduzi wa
programu hiyo inayofahamika kama Albinism Sports & Culture Tour utafanyika  Jumapili ya Septemba 29, katika viwanja vya
Serengeti Mjini Tarime .
Katibu wa Mkuu wa Albinism Sports Club  Joseph Sinda  amesema 
timu za mpira wa miguu  za watu
wenye ualbino kutoka DR Congo na Kenya 
zitashiriki katika uzinduzi wa programu hiyo .
“  Lengo la
programu hii ni kuongeza uelewa juu ya ualbino lakini pia kuhamasisha jamii
kuweza kutushirikisha katika shughuli za kiuchumi, kijamii na kisiasa .
Tutafanya hayo kapitia michezo na sanaa ambazo zinafanywa na watu wenye
ualbino”, Sinda  aliwaambia waandishi wa
habari mjini Tarime jana.
Sinda alisema programu hiyo itahusisha uendeshaji wa
harambee  mbalimbali kuchangisha  fedha kwa ajili ya kuanzisha miradi ya
kiuchumi  ambayo itasadia  kuhudumia 
watu wenye ualbino .
 Mfano Sinda
ambaye pia ni mwenyekiti wa watu wenye ualbino Wilaya ya Tarime alisema wana
mpango wa kuanzia kiwanda cha kuzalisha mafuta ya alizeti.
Aidha Sinda amesema 
programu hiyo  itasadia kukuza
utalii wa ndani .
“ Progamu hii itazinduliwa Tarime na mara baada ya
uzinduzi tutatembelea  mbuga mbalimbali .
Tutaanza kutembelea hifadhi ya taifa ya Serengeti kwa uwezesho wa shirika la
hifadhi za taifa (TANAPA)”, alisema Sinda.
TAZAMA VIDEO :
“


No comments:
Post a Comment