Na Mwandishi wetu,
Charles George Waitara leo October 1, 2019 amekabidhi msaada
wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 60 katika Hospitali ya
Wilaya ya Tarime .
Vifaa hivyo ni Biochemistry Mashine, magodoro 180 na
kompyuta tisa.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa Wilaya ya Tarime,
Charles George Waitara msaada umetolewa
na ubalozi wa China nchini Tanzania
baada ya kukubali ombi lake kwa lengo la kuboresha huduma za afya
katika hospitali hiyo ambayo inahudumia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Tarime
na Wilaya jiirani za Mkoa wa Mara.
Waitara amesema msaada huo pia umelenga kuunga mkono kazi
nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli
kuboresha huduma za jamii kwa wananchi.
“ Kama mwananchi wa kawaida
niliona nijitose kutafuta vifaa hivi ili kumuunga mkono mheshimiwa Rais
ambaye anafanya mambo makubwa katika taifa letu” amesema Charles George
Waitara.
Akipokea msaada huo , Mkuu mpya wa Wilaya ya Tarime Mhandisi
Mtemi Msafiri amemshukuru Charles George
Waitara kwa msaada huo na kutoa wito kwa watu wengine kuiga mfano wake.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias
Ntiruhungwa amesema msaada huo umeifanya
Hospitali hiyo kwa mara ya kwanza kuwa na kifaa cha Biochemestry machine ambacho
kinatoa huduma za figo, maini na moyo.
“ Kitendo alichokifanya leo ndugu yetu Charles George Waitara
ni cha kizalendo sana na hii mashine ya
Biochemestry itaanza kutoa huduma katika hospitali yetu leo”, amesema Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya
Mji wa Tarime.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr Calvin Mwasha amesema vifaa
hivyo vitawasadia kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa.
Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi wa hospitai hiyo John
Daniel Chomete amewataka watumishi wa hospitali hiyo kutumia vizuri vifaa hivyo.
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa
Mara Samwel Kiboye Namba Tatu na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime Charles Francis Kabeho ambaye kwa sasa ni
Mkuu wa Wilaya ya Chato .
No comments:
Post a Comment