NEWS

Tuesday 1 October 2019

CHARLES GEORGE WAITARA ATOA MSAADA WA VIFAA HOSPITALI YA TARIME


Na Mwandishi wetu,
Charles George Waitara leo October 1, 2019 amekabidhi msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 60 katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime .
Vifaa hivyo ni Biochemistry Mashine, magodoro 180 na kompyuta tisa.
Akikabidhi vifaa hivyo kwa viongozi wa Wilaya ya Tarime, Charles George Waitara  msaada umetolewa na ubalozi wa China nchini Tanzania  baada ya kukubali  ombi  lake kwa lengo la kuboresha huduma za afya katika hospitali hiyo ambayo inahudumia mamia ya wananchi wa Wilaya ya Tarime na Wilaya jiirani za Mkoa wa Mara.
Waitara amesema msaada huo pia umelenga kuunga mkono kazi nzuri inayofanywa na serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli kuboresha huduma  za jamii kwa wananchi.
“ Kama mwananchi wa kawaida  niliona nijitose kutafuta vifaa hivi ili kumuunga mkono mheshimiwa Rais ambaye anafanya mambo makubwa katika taifa letu” amesema Charles George Waitara.

Akipokea msaada huo , Mkuu mpya wa Wilaya ya Tarime Mhandisi Mtemi Msafiri  amemshukuru Charles George Waitara kwa  msaada huo na  kutoa wito kwa watu wengine kuiga mfano  wake.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime Elias Ntiruhungwa amesema  msaada huo umeifanya Hospitali hiyo kwa mara ya kwanza kuwa na kifaa cha Biochemestry machine ambacho kinatoa huduma za figo, maini na moyo.

“ Kitendo alichokifanya leo  ndugu yetu Charles George Waitara ni cha kizalendo sana  na hii mashine ya Biochemestry itaanza kutoa huduma katika hospitali yetu leo”, amesema Mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya Mji wa Tarime.
Mganga Mkuu wa Hospitali hiyo Dr Calvin Mwasha amesema vifaa hivyo vitawasadia kuboresha huduma za matibabu kwa wagonjwa.

Kwa upande wake mwenyekiti wa bodi wa hospitai hiyo John Daniel Chomete amewataka watumishi wa hospitali  hiyo kutumia vizuri vifaa hivyo.
 
Hafla hiyo pia imehudhuriwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Samwel Kiboye Namba Tatu na   aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Tarime  Charles Francis Kabeho ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Wilaya ya Chato .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages