NEWS

Monday 13 January 2020

HISTORIA YAWEKWA: GAZETI LA KWANZA LAZINDULIWA MKOA WA MARA +VIDEO


Mkuu wa Wilaya ya Tarime Eng Mtemi Msafiri leo Januari 13,2020 amezindua gazeti la Sauti ya Mara kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Mara (RC) Adam Malima.

Toleo la kwanza la gazeti hilo  ambalo litakuwa likitoka  kila siku ya Jumatatu  limetoka leo na limesambazwa katika mikoa ya kanda ya Ziwa ukiwemo Mkoa wa Mwanza. Gazeti hilo limeanzishwa na kampuni ya Mara Online.
Eng Msafiri amesema RC Malima amefurahishwa  sana na uanzishwaji wa gazeti hilo  hususani ni kauli mbiu yake ambayo ni Habari kwa Maendeleo .

“ Ni imani yetu kuwa gazeti hili litakuwa chachu ya maendeleo ya mkoa wa Mara “, amesema Eng Msafiri ambaye alifuatana na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wa wilaya ya Tarime.

Viongozi mbalimbali kutoka chama cha CCM na CHADEMA wakiwemo wawakilishi wa wabunge wa jimbo la Tarime Mjini na jimbo la Tarime  vijijini, wadau wa maendeleo na viongozi wadini wamehudhuria  uzinduzi huo ambao umefanyika katika Hoteli ya Goldland.
Mtendaji Mkuu wa Mara Online Jacob Mugini amesema gazeti mbali litakuwa likitoa habari ambazo zinahamasisha maendeleo na uhifadhi endelevu litakuwa na ukurasa maalumu kwa ajili ya kuonesha uzuri wa Mkoa wa Mara .

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages