HALMASHAURI ya Wilaya ya
Serengeti mkoani Mara kupitia hospitali ya wilaya hivi sasa inawafanyia vipimo
vya joto abiria wa mabasi na magari ya
watu binafsi wanaoingia na kutoka wilayani humo kupitia Hifadhi ya Taifa ya
Serengeti.
Mkurugenzi wa Halmashauri
ya Wilaya ya Serengeti Mhandisi Juma Hamsini amesema mpango huo utakuwa
endelevu kipindi hiki cha janga la Corona kuhakikisha usalama wa afya za abiria
wanaosafiri kupitia ndani ya hifadhi hiyo kuelekea Ngorongoro, Manyara, Karatu
na Arusha.
No comments:
Post a Comment