NEWS

Thursday 16 April 2020

DC Serengeti : Wananchi wetu wameitikia wito kupambana na Corona

Mkuu wa wilaya ya Serengeti Nurdin Babu (wa tatu kushoto) akiendelea na zoezi la kutoa elimu juu ya kujikinga na virusi vya Corona kwa wananchi 
Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Nurdin Babu amesema wananchi wa wilaya hiyo wameitikia wito wa kuchukua tahadhari  dhidi ya COVID -19 “ Kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya yetu , Mkurugenzi(DED), mganga mkuu(DMO) tayari tumefanya ziara katika kata 17 kuhamasisha wananchi kuchukua tahadhari dhidi ya Corona na wameitikia vizuri sana kwa kufuata maelekezo ya wataalamu . Mfano wameka ndoo za kuna mikono maeneo mengi sana“, amesema Mkuu huyo wa Wilaya.
Amesema zoei hilo la kutoa elimu kwa wananchi kuendelea kujikinga na virusi vya Corona linaendelea katika maeneo mengine.
Vita dhidi ya Corona: Abiria ambao walikuwa wakisafiri kutoka Arusha wakipimwa  joto kwa kutumia kifaa maalumu cha “ Infrared Thermometer”,  katika geti la Ikoma Wilaya ya 
Serengeti  Mkoani Mara hivi karibuni. Mojawapo ya dalili za COVID-19 ni mgonjwa kuwa 
na kiwango kikubwa cha joto ( zaidi ya 38*C. ( picha na mpiga picha wetu).

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages