Raisi wa Afrika Kusini ,Cyril Ramphosa
ampa Waziri Stella Ndabeni Abrahams likizo ya miezi miwili ,mwezi mmoja ukiwa
wa bila malipo baada ya kukiuka agizo la kujitenga na kukaa ndani kufuatia
mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Corona kuenea kwa kasi nchini humo na
kupelekea Raisi kutoa agizo la kila mwananchi kukaa ndani kujilinda dhidhi ya
maambukizi.
Kama ilivorushwa katika mitandao
ya kijamii Waziri huyo mwenye dhamana katika idara ya mawasiliano nchini mapema siku hiyo alimtembelea rafiki yake kwa
ajili ya chakula cha mchana hivyo kukiuka agizo la kutotembeleana na kukaa
nyumbani kama alivyoagiza Raisi.
Kutokana na ongezeko la
maambukizi ya virusi vya corona nchini Afrika ya Kusini wananchi wamekatazwa
kutoka ndani ya nyumba zao na kutakiwa kukaa nyumbani tu na yoyote anaekikuka
agizo hilo anakamatwa.
No comments:
Post a Comment