NEWS

Wednesday 8 April 2020

RAIS WA AFRIKA KUSINI AMSHIKISHA ADABU WAZIRI KWA KUKIUKA MASHARTI YA KUJIKINGA NA CORONA



       Raisi wa Afrika Kusini ,Cyril Ramphosa ampa Waziri Stella Ndabeni Abrahams likizo ya miezi miwili ,mwezi mmoja ukiwa wa bila malipo baada ya kukiuka agizo la kujitenga na kukaa ndani kufuatia mlipuko wa ugonjwa wa Virusi vya Corona kuenea kwa kasi nchini humo na kupelekea Raisi kutoa agizo la kila mwananchi kukaa ndani kujilinda dhidhi ya maambukizi.
     Kama ilivorushwa katika mitandao ya kijamii Waziri huyo mwenye dhamana katika idara ya mawasiliano nchini  mapema siku hiyo alimtembelea rafiki yake kwa ajili ya chakula cha mchana hivyo kukiuka agizo la kutotembeleana na kukaa nyumbani kama alivyoagiza Raisi.
     Kutokana na ongezeko la maambukizi ya virusi vya corona nchini Afrika ya Kusini wananchi wamekatazwa kutoka ndani ya nyumba zao na kutakiwa kukaa nyumbani tu na yoyote anaekikuka agizo hilo anakamatwa.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages