NEWS

Sunday 10 May 2020

Mwanamke atendewa uonevu wa kutisha, DC atoa tamko

MKUU wa Wilaya (DC) ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri, amekemea kitendo cha kufywekwa kwa shamba la migomba/ndizi la mwanamke Angelina Mwita kilichofanywa na ndugu wa mume wake.

Aidha, Mhandisi Msafiri ametaka hatua kali za kisheria zichukuliwe haraka dhidi ya waliohusika kutenda uovu huo.

Mkuu huyo wa wilaya ameyasema hayo jana Mei 9, 2020 alipofika na kushuhudia uharibifu mkubwa wa shamba hilo katika kijiji cha Ntagacha.

Mhandisi Msafiri akionekana kushitushwa na uharibifu wa migomba ya Angelina Mwita

Taarifa zinasema kumekuwepo na mgogoro wa muda mrefu kati ya Angelina na ndugu wa kiume wa mume wake na kumweka mwanamke huyo katika wakati mgumu wa kuhudumia familia yake ya watoto kadhaa.

Angeina Mwita(katikati) na watoto wake wakiwa katika shamba lao baada ya kufyekwa

Mkuu wa Wilaya huyo amekuwa akikemea vitendo vya ukatalii na unyanyasaji wa kijinsia katika wilaya hiyo huku vita hiyo ikipata msukumo mkubwa kutoka kwa mkuu wa Mkoa wa Mara (RC) Adam Malima.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages