FAMILIA
kadhaa wilayani Rorya zimeondoa matumaini ya kuvuna mazao ya chakula baada ya
kuamka leo Ijumaa asubuhi na kukuta mashamba
yao yamesombwa na mafuriko ambayo yalisbabisha korongo.
Tukio
hilo limetokea katika kitongoji cha Dagopa, kijiji cha Nyambogo katani Kitembe.
Wakulima wakitazama mashamba yao bila mazao |
“
Tunaona kama kumetokea mlipuko fulani
ambao umeacha korongo baada ya kusomba mazao kwenda mtoni. Tumeamka asubuhi
tumekuta mashamba hayapo,” Mmoja wa waathirika wa maafa hayo, Denis William,
alisema ameambia Mara Online News leo asubuhi.
Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dogopa, Mathew
Madoye,
amesema
mashamba mengi ya mahindi, miwa, mihogo
na mtamo yamesombwa.
Kwa
mujibu wa Madoye, kaya zaidi ya 40 zimeathirika kutokana na maafa hayo.
(
Habari ,Picha na Mwandishi wetu Rorya)
No comments:
Post a Comment