NEWS

Friday 1 May 2020

Pigo kwa wakulima Rorya



FAMILIA kadhaa wilayani Rorya zimeondoa matumaini ya kuvuna mazao ya chakula baada ya kuamka leo Ijumaa asubuhi na kukuta  mashamba yao yamesombwa na mafuriko ambayo yalisbabisha korongo.

Tukio hilo limetokea katika kitongoji cha Dagopa, kijiji cha Nyambogo katani Kitembe.

Wakulima wakitazama mashamba yao bila mazao 

“ Tunaona kama kumetokea  mlipuko fulani ambao umeacha korongo baada ya kusomba mazao kwenda mtoni. Tumeamka asubuhi tumekuta mashamba hayapo,” Mmoja wa waathirika wa maafa hayo, Denis William, alisema ameambia Mara Online News leo asubuhi.
 
Sehemu ya korongo iliyojitokeza katika eneo la tukio
 Mwenyekiti wa Kitongoji cha Dogopa, Mathew Madoye,
amesema  mashamba mengi ya mahindi, miwa, mihogo na mtamo yamesombwa.
 
Mmoja wa wahanga akinyanyua mazao ya mahindi
Kwa mujibu wa Madoye, kaya zaidi ya 40 zimeathirika kutokana na maafa hayo.

( Habari ,Picha na Mwandishi wetu Rorya)


No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages