MKUU
wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Simon Sirro, amewataka wanasiasa
kufanya kazi zao kwa kufuata na kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za
nchi bila kuingilia shughuli za kiutendaji za jeshi hilo.
IGP Sirro akiwatunuku vyeo Askari Polisi mkoani Simiyu |
IGP Sirro ameyasema hayo Juni 3, 2020 wakati wa ziara yake ya kikazi mkoani Simiyu na kuongeza kuwa jeshi hilo halitawaingilia wanasiasa kwenye shughuli zao endapo hawatavunja sheria.
Amesisitiza kuwa jeshi hilo halitawavumilia wanasiasa wanaotumia nafasi zao kwenye vyama vya siasa kuingilia majukumu ya vyombo vya ulinzi na usalama.
Kamanda Sirro amewakumbusha wanasiasa watambua kuwa wanaendesha shughuli zao kwa sababu kuna amani na kwamba amani ikitoweka hawawezi kuziendesha, hivyo waliache jeshi hilo lifanye kazi yake kwa mujibu wa sheria za nchi.
IGP Simon Sirro akizungumza na askari polisi mkoani Simiyu |
Askari waliotunukiwa cheo cha koplo, G 8018 Koplo Maiko Luvanda (kulia) na H 742 Koplo Paulo Komba |
(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi)
No comments:
Post a Comment