Mwalimu wa Shule ya
Msingi Azimio ya mjini Tarime mkoani Mara, Richard Leonce amefariki dunia,
huku mke na mtoto wake wakijeruhiwa vibaya kwa ajali ya moto iliyotokea
nyumbani kwao leo Jumatano Juni 10, 2020, saa nne asubuhi.
Diwani wa Kata ya Bomani,
Masubo Nkori na Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa National, Bernard Nyagiro
wameiambia Mara Online News kwamba mke wa Mwalimu Leonce, Happiness Mnisi
ambaye ni mwalimu wa Shule ya Msingi Remagwe na mtoto wao wa kike, Bright,
wamelazwa kwa matibabu katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime.
Mwalimu Richard Leonce wakati wa uhai wake |
Kwa mujibu wa viongozi
hao, chanzo cha ajali hiyo ya moto kinaweza kuwa hitilafu ya umeme ndani ya
nyumba yao iliyopo eneo la National Housing mjini Tarime.
Kamanda wa Polisi Tarime
Rorya, ACP William Mkonda, amethibitisha na kusema jeshi hilo limeanza
uchunguzi wa kubaini chanzo halisi cha ajali hiyo ambayo pia imeteketeza mali
mbalimbali zilizokuwa ndani ya nyumba ya familia hiyo.
(Imeandikwa na Samsn Chacha, Tarime)
Kwa kweli nimeshtushwa sana na taà rifa ya ajali ya moto iliyosababosha Kifo cha rafiki yangu Mwl. Rich!
ReplyDeleteEe Mungu, utusaidie! Uwaponye majeruhi ( Mama na mwanawe)
Àmen!