Mwenyekiti UVCCM Chuo cha Ushirika Moshi,
Mwita Mhorere avuta fomu ubunge Serengeti
MWENYEKITI wa Umoja wa
Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi, Mwita
Simion Mohere, leo Julai 14, 2020 amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania ubunge
katika jimbo la Serengeti mkoani Mara.
Akizungumza na Mara Online
News mara baada ya kuchukua fomu hiyo katika ofisi ya CCM Wilaya, Mohere
amesema anahitaji kulistawisha kiuchumi jimbo la Serengeti ambalo anasema
limekuwa nyuma kimaendeleo kutokana na kukosa mbunge mwenye uwezo na utashi wa
kuwatumikia wananchi kwa kiwango kinachoridhisha.
“Serengeti tumekuwa nyuma
kimaendeleo, nimeona nina uwezo na uzoefu wa uongozi, hivyo ninahitaji kuwa
miongoni mwa viongozi wanaokwenda na kasi ya Rais Dkt John Pombe Magufuli
katika kuwaletea wananchi maendeleo ya kweli, mimi ni mtu sahihi, kwa uzoefu na
uwezo wangu nina uhakika wa kuleta mabadiliko Serengeti,” amesisitiza Mohere.
hakika huyu ndio mtu sahihi wa kulikomboa jimbo letu
ReplyDelete