MKURUGENZI wa Professor Mwera Foundation, Hezbon Peter Mwera(kulia),
amekuwa mwanachama wa kwanza wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuchukua fomu ya
kuwani ubunge katika Jimbo la Tarime Mjini, leo asubuhi Julai 14, 2020.
Kada huyo kijana na msomi wa chuo kikuu, amesema uwezo na uzoefu
wake katika uongozi ndivyo vimemsukuma kuwania ubunge ili atumie nafasi hiyo
kuharakisha maendeleo ya Tarime Mjini kwa kuhuisha miradi ya kijamii
iliyosimama, kuboresha iliyopo na kuongeza mipya kwa manufaa ya wakazi wa jimbo
hilo.
Mwanachama wa CCM aliyemfuatia Mwera kuchukua fomu ya
kinyang'anyiro hicho katika ofisi ya chama hicho wilaya ya Tarime ni Jackson
Christopher Kangoye.
(Imeandikwa na Mara Online News)
No comments:
Post a Comment