NEWS

Saturday 8 August 2020

Simiyu kuunganishwa na Hospitali ya Taifa Muhimbili

Muonekano wa sehemu ya majengo ya Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu.
 

NAIBU Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt Godwin Mollel, amesema wizara hiyo inakusudia kuiunganisha Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu na Hospitali ya Taifa Muhimbili ili kurahisisha huduma za matibabu kwa wagonjwa.

 

Dkt Mollel ameyasema hayo Agosti 7, 2020 mara baada ya kukagua ujenzi wa mradi wa jengo la mama na mtoto katika hospitali ya hiyo iliyopo Nyaumata mjini Bariadi, Simiyu.

Naibu Waziri, Dkt Godwin Mollel (katikati), Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt Festo Dugange (kulia) na Mganga Mfawidhi wa hospitali hiyo, Dkt Matoke Muyenjwa (kushoto), wakati wa ziara ya waziri huyo hospitalini hapo.

Amesema kabla ya ujenzi wa hospitali hiyo, wagonjwa walikuwa wakilazimika kutumia gharama kubwa kusafiri umbali mrefu kwenda kutafuta matibabu katika Hospitali ya Rufaa Bugando jijini Mwanza, lakini kwa sasa wanapata huduma kwa urahisi mkoani hapa.

 

Awali, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt Festo Dugange, amesema kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita chini ya uongozi wa Rais Dkt John Pombe Magufuli, vituo vya afya vimeongezeka kutoka 196 hadi 218 sawa na ongezeko la asimilia zaidi ya 40, hali ambayo imepunguza vifo vya kinamama na watoto wachanga.

Sehemu ya ujenzi wa jengo la wodi unaoendelea katika Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu.
 

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Simiyu, Dkt Matoke Muyenjwa, amesema wametenga Sh milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa vifaa tiba.

 

(Imeandikwa na Anita Balingilaki, Bariadi)

1 comment:

  1. Habari njema hiyo kwa watu wa kanda ya ziwa kwa ujumla

    ReplyDelete

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages