NEWS

Monday 28 September 2020

Lissu: Nina imani na wapigakura Tarime Mjini

Mgombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu  (kushoto) na mgombea ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia chama hicho, Esther Matiko (kulia) wakiwapungia wananchi kwenye mkutano wa kampeni mjini Tarime, jana Jumapili jioni. (Na Mpigapicha Wetu)


 

MGOMBEA urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu amesema ana imani na wapigakura wa jimbo la Tarime Mjini kuwa watakipatia ushindi chama hicho katika uchaguzi mkuu ujao.

 

“Nina imani na nyie kuwa mtatimiza wajibu wenu. Tupeni kura nyingi zaidi,” Lissu amesema wakati akihutubia mkutano wake wa kampeni mjini Tarime, jana Jumapili jioni.

Wananchi wakifuatilia hotuba ya ngombea urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chadema, Tundu Lissu (hayupo pichani) katika mkutano wa kampeni uliofanyika mjini Tarime, jana Jumapili jioni.

 

Awali, katika mkutano huo, mgombea ubunge Tarime Mjini kupitia Chadema, Esther Matiko amewaomba wananchi wa jimbo hilo kumchagua kwa mara ya pili huku akijitetea kuwa hakuhusika na ubomoaji wa soko la zamani la Tarime mjini.

 

Katika kinyang’anyiro hicho, Matiko anachuana na Michael Kembaki anayegombea nafasi hiyo kwa tiketi ya CCM na Mary Nyagabona (NCCR – Mageuzi).

 

(Imeandikwa na Mara Online News)

 

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages