NEWS

Monday 14 December 2020

Uzinduzi Baraza la Madiwani Tarime Mji katika picha

 

Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (katikati), Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, John Marwa (kulia) na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa (kushoto) wakiwa makini kwa ajili ya kuanza kuimba Wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.  


Mbunge wa Tarime Mjini, Michael Kembaki (kulia), Mwenyekiti mpya wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (wa tatu kushoto), Katibu Tawala Wilaya ya Tarime, John Marwa (wa tatu kulia), Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa (wa pili kushoto) na viongozi wengine wakiimba Wimbo wa Taifa mara baada ya madiwani kula viapo mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.


Maofisa wa vyombo vya Ulinzi na Usalama wakiungana na wengine kuimba Wimbo wa Taifa wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Ghatty Zephania Chomete akila kiapo ili kuwa Mjumbe wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime wakati wa uzinduzi wa Baraza hilo mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.


Diwani wa Kata ya Kenyamanyori, Farida Joel Nchagwa akila kiapo wakati wa uzinduzi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye ukumbi wa MCN, leo Desemba 14, 2020.


Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa (kushoto) na viongozi wengine wakifuatilia viapo vya madiwani wa Halmashauri hiyo kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.Wawakilishi wa taasisi mbalimbali na vyama vya siasa wakifuatilia uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.


Wananchi wakifuatilia viapo vya madiwani wakati wa uzinduzi wa Baraza jipya la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.


Sehemu ya wananchi wakifuatilia uzinduzi wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Mji wa Tarime kwenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.


Madiwani wateule wa Halmashauri ya Mji wa Tarime wakisikiliza maelekezo ya Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo, Elias Ntiruhungwa, kabla ya kula kiapo kenye ukumbi wa MCN mjini Tarime, leo Desemba 14, 2020.

Habari picha zote na Mara Online News

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages