|
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (mwenye kofia katikati), Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga (kushoto), Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri (wa pili kusshoto), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (wa tatu kushoto), Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (kulia), Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online, Jacob Mugini (wa pili kulia) na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Thobias Ghati wakipiga na kushangilia baada ya mtoto Angel Jacob Mugini kukata utepe wa uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020.
|
HISTORIA ya aina yake imeandikwa kwa kushuhudiwa uzinduzi wa
chombo cha habari cha kidijitali ambacho ni Blogu ya Mara Online News,
uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, vyama vya siasa na wadau wa
uhifadhi wa wanyamapori, vyanzo vya maji na mazingira.
|
Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (aliyesimama) akihutubia katika uzinduzi
wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020.
Waliokaa kutoka kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Tarime, Mhandisi Mtemi
Msafiri, Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete na Ofisa Mtend.aji Mkuu wa Mara Online, Jacob Mugini.
|
Hafla ya uzinduzi huo uliofana kwa aina yake imefanyika leo
Desemba 15, 2020 katika viwanja vya ofisi ya Taasisi ya Mara Online inayomiliki
Blogu hiyo na Gazeti la Sauti ya Mara.
|
Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima (kushoto) akipokea zawadi ya kalenda maalumu ya uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020. Anayemkabidhi ni Ofis Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Mara Online inayomiliki blogu hiyo.
|
|
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online, Jacob Mugini (kulia) akimkabidhi Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete zawadi ya kalenbda maalumu ya uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News, leo Desemba 15, 2020.
|
Viongozi wa Serikali waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mkuu
wa Mkoa wa Mara, Adam Malima aliyekata utepe wa uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya
Tarime, Mhandisi Mtemi Msafiri, Mkuu wa Wilaya ya Rorya, Simon Odunga, Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete aliyekuwa mgeni rasmi na Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote.
|
Baadhi ya wadau walioshiriki hafla ya uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020. |
|
|
Wawakilishi wa Grumeti Fund, Cecilia Benizeti (kushoto) na David Mwakipesile (anayemfuatia) wakifuatilia uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020.
|
|
Mwakilishi wa Idara ya Ujirani Mwema ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Zabron Mtweve (kushoto) akipokeza zawadi ya kalenda kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mara, Ghatty Chomete wakati wa uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini Tarime, leo Desemba 15, 2020. Kulia ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online inayomiliki blogu hiyo.
|
Baadhi ya wadau wa uhifadhi waliohudhuria ni Zabron Mtweve
kutoka Idara ya Ujirani Mwema ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi Kanda ya Magharibi, Martin Loiboki kutoka TANAPA, David
Mwakipesile na Cecilia Benizeti kutoka Grumeti Fund, Mwita Seri na Siproza
Charles kutoka jumuiya za watumia maji kanda za Tigite Chini na Mara Kaskazini, Peter kutoka Kituo cha Maendeleo ya Kilimo Mogabiri.
|
Mbunge
wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (kushoto) akimkabidhi
Mkurugenzi wa Kampuni Kemange Investment, Jumanne Jackson Karomba zawadi
ya kalenda maalumu ya uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News mjini
Tarime, leo Desemba 15, 2020. |
Washiriki wengine ni madiwani, wafanyabishara,
maofisa wa vyombo vya ulinzi na usalama, wawakilishi wa benki za CRDB na NMB Tarime, wafanyakazi wa Mara Online na
waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali vya habari mkoani Mara.
|
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Chomete (wa pili kulia waliokaa) ambaye amekuwa mgeni Rasmi wa Uzinduzi wa Blogu ya Mara Online News leo Desemba 15, 2020. Wengine ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mara Online inayomiliki blogu hiyo, Jacob Mugini (aliyekaa kulia), Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Daniel Komote (wa pili kushoto) na Makamu wake, Thobias Ghati. Waliosimama ni wafanyakazi wa Mara Online News akiwemo Mhariri Mkuu, Christopher Gamaina (kulia).
|
(Habari na picha zote na Mara Online News)
Keep it up, Mara Online na wanahabari wake wote, this is amazing Idea and innovative one in Lake zone.
ReplyDeleteTuko pamoja kuipeleka Blogu yetu Mbele kama wadau na Watumiaji wa mfumo wa kidijitali. Tunajivunia Ninyi 👊👊👊👊👊👊 C.E.O Brother Jacob Mugini na Team yako wote.
Mungu awape maarifa makubwa zaidi.