NEWS

Saturday 30 January 2021

Mfahamu bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani

Kylie Jenner

KYLIE Jenner amekuwa bilionea mwenye umri mdogo zaidi duniani hadi sasa, kwa mujibu wa orodha ya mabilionea iliyopo kwenye jarida maarufu ulimwenguni la Forbes.

 

Kylie ambaye ndiye mdogo zaidi katika familia ya Kardashian amepata utajiri wake kutokana na biashara ya vipodozi.

Kylie Jenner

Akiwa na umri wa miaka 21 mwaka 2018 alikuwa ameshaanzisha na hadi sasa anamiliki kampuni ya vipodozi ya Kylie Cosmetics, biashara ya urembo ambayo imedumu kwa miaka minne sasa na kuingiza mapato ya takriban Dola za Kimarekani milioni 360 mwaka huo.

 

Alifikia mafanikio haya mapema kuliko mwasisi wa mtandao wa kijamii wa Facebook Mark Zuckerberg ambaye alikuwa bilionea akiwa na umri wa miaka 23.

Kylie Jenner

Sikutarajia chochote. Sikujua hali ya baadae. Lakini kutambuliwa inafurahisha. Ni jambo zuri la kunitia moyo,” Kylie aliliambia jarida la Forbes.

 

Orodha ya Forbes inaonesha mwasisi wa The List Shows Amazon, Jeff Bezos, akiendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwa binadamu tajiri zaidi duniani.

Kylie Jenner

Jumla ya utajiri wake ni Dola bilioni 131, kulingana na jarida la Forbes, ameongeza hadi Dola bilioni 19 kutoka mwaka 2018.

 

Lakini kiwango cha mapato ya mabilionea wote kwa ujumla kimeshuka kutoka Dola trilioni 9.1.

Kylie Jenner

Miongoni mwa mabilionea ambao utajiri wao unapungua ni mwanzilishi wa Facebook Mark Zuckerberg.

 

Umeshuka kwa Dola bilioni 8.7 katika kipindi cha mwaka uliopita ulishuka kwa Dola bilioni 62, kwa mujibu wa orodha iliyopo jarida la Forbes.

Kylie Jenner
 

Hisa zake katika Facebook wakati mmoja zilipungua kwa thamani ya theluthi moja wakati kampuni ilipokuwa ikikabiliana na kashfa.

 

Hisa za kampuni ya mauzo ya mtandaoni ya Amazon zimefanya vizuri na hivyo kuboresha akaunti za benki za Bezos na mwanya kati yake na Bill Gates, ambaye yupo katika nafasi ya pili, ingawa utajili wa Gates umepanda hadi Dola bilioni 96.5 kutoka Dola bilioni 90 alizokuwa nazo mwaka juzi.

Kylie Jenner

Kwa mabilionea wote waliotajwa kwenye orodha hiyo, mwanamke tajiri zaidi aliyejitafutia utajiri mwenyewe ni Mogul Wu Yajun wa nchini China kupitia kampuni yake - akiwa na utajiri wenye thamani ya takriban Dola bilioni 9.4.

 

Idadi ya wanawake waliojitafutia utajiri wao imeongezeka kwa mara ya kwanza na kufikia hadi wanawake 72 kutoka wanawake 56 mwaka juzi

Kylie Jenner na mwanaye

Jarida la Forbes hutumia viwango vya bei katika masoko ya hisa vya siku hiyo na viwango vya mauzo ya fedha kutoka kote duniani.

 

Kulingana na Forbes, kuna mabilionea wachache wapatao 2,153, miongoni mwao wakiwa katika orodha ya mwaka 2019, kiwango hicho kikiwa kimeshuka ambapo mwaka 2018 walikuwa 2,208.

Kylie Jenner na mwanaye
 

Forbes pia lilibaini kwamba katika mabilionea 994, miongoni mwao hali ya utajiri sio nzuri ikilinganishwa na mwaka juzi.

 

Luisa Kroll, ambaye ni Naibu Mhariri wa masuala ya utajiri katika jarida la Forbes, amesema “Hata nyakati za mtikisiko wa uchumu na rasilimali mjasiriamali hupata njia za kupata utajiri.”

Kylie Jenner

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages