NEWS

Friday 29 January 2021

Mafuriko yakwamisha wachimbaji wadogo mgodi wa Msege

Mojawapo ya mashimo ya wachimbaji wadogo wa dhahabu yaliyojaa maji katika mgodi wa Msege wilayani Tarime, Mara.

 

WACHIMBAJI wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Msege uliopo Tarime mkoani Mara wamesimama kuendelea na shughuli hizo baada ya mashimo husika kukumbwa na mafuriko.

 

“Tumeingia hasara kubwa sana, tumetumia pesa nyingi kuwekeza lakini sasa mashimo yetu yamejaa maji,” amesema Elias Nyansika katika mazungumzo na Mara Online News wilayani Tarime, hivi karibuni.

 

Nyansika ni mmoja wa wachimbaji wadogo wa dhahabu katika mgodi wa Msege ambao umekuwa na fursa za ajira kwa vijana wengi.

 

Wachimbjai hao wameiomba Serikali kupitia Wizara ya Madini kuwaangalia kwa jicho la msaada, hasa katika kipindi hiki cha mafuriko kwenye mgodi huo.

 

Pia wameomba huduma ya umeme kwa ajili ya kuendesha mitambo ya kuvuta maji yaliyojaa kwenye mashimo yao.

 

Wilaya ya Tarime ni miongoni mwa maeneo ya mkoa wa Mara yenye idadi kubwa ya wachimbaji wadogo wa madini.

 

Mara Online News inaendelea kutafuta idadi halisi ya wachimbaji wadogo walioathirika katika eneo hilo kutokana na mafuriko hayo.

 

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages