NEWS

Wednesday 13 January 2021

TRA yaelimisha wafanyabiashara Serengeti uwasilishaji ritani kwa njia ya mtandao

Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Mwandamizi wa TRA Mkoa wa Mara, Zake Wilbard Rwiza.

MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA) Mkoa wa Mara imeendesha semina ya kuwaelimisha wafanyabiashara mbalimbali katika wilaya ya Serengeti kuhusu uwasilishaji wa ritani kwa njia ya mtandao (E Filling).

Baadhi ya washiriki wakimakinika katika semina hiyo.

Semina hiyo imefanyika kwenye ukumbi wa Hoteli ya Giraffe Garden mjini Mugumu leo Januari 13, 2021, ambapo imewezeshwa na Afisa Elimu na Huduma kwa Mlipakodi Mwandamizi wa TRA Mkoa wa Mara, Zake Wilbard Rwiza kwa kusaidiana na Meneja wa TRA Wilaya ya Serengeti, Titus Shindano,

Mfanyabiashara Paul Magoiga ni miongoni mwa washiriki wa semina hiyo.

Pamoja na mambo mengine, Rwiza amewaelimisha wafanyabiashara hao namna ya kuingia kwenye mtandao, kujaza fomu husika na kuwasilisha ritani zao TRA.

 

Amesema lengo la mfumo huo ni kumrahisishia mteja kulipa kodi akiwa mahali popote, lakini pia kuwezesha Serikali kukusanya mapato yake kwa wakati kupitia TRA.

Sehemu nyingine ya washiriki wakifuatilia mada katika semina hiyo.

Rwiza ametaja faida ambazo wafanyabiashara watazipata kutokana na kuwasilisha ritani kwa njia ya mtandao kuwa ni pamoja na wepesi wa kuutumia na kujikadiria wenyewe kiasi cha kulipa kutokana na mapato yao.

Meneja wa Hoteli ya Giraffe Garden, Adolf Sylvester akifurahia jambo wakati wa semina hiyo.

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages