NEWS

Thursday 7 January 2021

Waziri Aweso aagiza Mhandisi Masanja akamatwe

Waziri wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso akiagiza Mhandisi Emmanuel Masanja akamatwe.

WAZIRI wa Maji, Jumaa Hamidu Aweso amemwomba Mkuu wa Mkoa wa Mara, Adam Malima kutumia vyombo vyake vya dola kumkamata Mhandisi Emmanuel Masanja kwa ajili ya kujibu tuhuma za kuhujumu miradi ya maji wilayani Rorya.

 

“Ninakuomba sana Mkuu wa Mkoa, huyu bwana akamatwe akatoe maelezo [kuhusu miradi iliyokwama licha ya wakandarasi husika kulipwa Sh zaidi ya bilioni moja lakini miradi husika haitoi maji],” amesema Waziri Aweso, leo Januari 7, 2021 kwenye kikao cha majumuisho ya ziara yake ya siku tatu katika wilaya za Tarime, Rorya na Musoma mkoani Mara.

 

Kwa mujibu wa Waziri Aweso, Mhandisi Masanja baada ya kuona ameboronga kwenye miradi ya maji wilayani Rorya alitaka kuhamishiwa mkoani Tabora.

 

“Mhandisi Emmanuel Masanja ndiye amekuwa akihujumu miradi yetu ya maji, baada ya kuharibu hapa akataka kuhamishiwa Tabora,” amesema Waziri Aweso na kumwambia Masanja “Tutakuchukulia hatua hata uwe na mapembe marefu kiasi gani, tutakushughulikia.”

Mhandisi Emmanuel Masanja akisikiliza agizo la kukamatwa kwake.

Baada ya agizo hilo la Waziri Aweso, Mkuu wa Mkoa, Malima, ameagiza maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na Jeshi la Polisi kumchukua Mhandisi Masanja kwa ahatua za mahojiano.

 

(Habari na picha zote na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages