NEWS

Wednesday 16 June 2021

Mbunge Ghati ahoji ujenzi wa barabara ya Tarime – Serengeti kwa kiwango cha lami



Mbunge Ghati Zephania Chomete akiwa bungeni

SERIKALI imesema itaendelea kujenga barabara ya Tarime - Serengeti kwa kiwango cha lami kadri inavyopata fedha.

Akijibu swali la Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete aliyetaka kujua ni lini barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami - leo asubuhi Juni 16, 2021, Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara amesema sehemu ya barabara hiyo yenye urefu kilomita 10.7 tayari imejengwa kwa kiwango cha lami.

Waitara ambaye pia ni Mbunge wa Tarime Vijijini, amesema kilomita 76.44 zilizobaki zitaendelewa kujengwa kwa kiwango cha lami kadri fedha inavyopatinana.
Waziri akijibu swali bungeni
 

Hata hivyo, Naibu Waziri huyo amesema Serikali imetenga bajeti ya Shilingi milioni 411 kwa ajili kuendelea kuboresha barabara hiyo kwa kiwango cha changarawe ili iweze kupitikika wakati wote.

Katika maswali yake ya nyongeza, Mbunge Ghati pia ametaka kujua mikakati ya Serikali ya kuhakikisha kuwa barabara hiyo inapitika kirahisi wakati wote.

Waitara ameongeza kuwa Serikali imejenga daraja la barabara hiyo la mto Mara linalounganisha wilaya za Tarime na Serengeti na barabara za maingilio ya daraja hilo pande zote mbili, zenye urefu wa kilomita 1.8, kwa kiwango cha lami.

Barabara hiyo inaelezwa kuwa inaweza kusadia kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijami, ikiwemo sekta ya utalii, endapo itajengwa kwa kiwango cha lami.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages