NEWS

Saturday 31 July 2021

Mbunge Matiko afunguka makubwa kuhusu maendeleo ya wana-Tarime
MBUNGE wa Viti Maalum wa Bunge la Tanzania, Esther Matiko (pichani juu) amefanya mahojiano na wahariri wa blogu ya Mara Online News na gazeti la Sauti ya Mara, na kuweka wazi namna anavyoendelea kushughulikia maendeleo ya wananchi wa jimbo la Tarime Mjini.

Katika mahojiano hayo maalumu yaliyofanyika nyumbani kwake mjini Tarime leo Julai 31, 2021 jioni, Mbunge Matiko amesema nafasi aliyonayo sasa, yaani ubunge wa viti maalum, bado imemwimarisha katika juhudi za kuwasemea na kuwaletea wananchi hao maendeleo makubwa ya kisekta, kuliko hata alivyokuwa mbunge wa jimbo hilo mwaka 2015 hadi 2020.

Mwanasiasa huyo ametumia nafasi hiyo kutaja miradi sita mikubwa ya maendeleo ya wana-Tarime, ambayo Serikali imeiingiza kwenye utekelezaji kutokana na jitihada, msukumo na ushawishi wake mkubwa bungeni na kwenye wizara husika.


Mbunge Matiko akizungumza bungeni

Makala maalumu kuhusu mahojiano hayo itachapishwa kwenye toleo la gazeti la Sauti ya Mara kesho kutwa Jumatatu, ikielezea kwa kina miradi mikubwa ya maendeleo ya wananchi wa Tarime, ambayo Mbunge Matiko ameipigania hadi imeanza kutekelezwa.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages