NEWS

Friday 23 July 2021

Safari ya kuwapokea nyumbu Serengeti yaiva, DC Tarime kushirikiDC Tarime, Col. Michael Mtenjele (kulia) na CEO Mara Online, Jacob Mugini: Tuko tayari kwa safari ya kuwapokea nyumbu Serengeti Jumapili.

OFISA Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Mara Online, Jacob Mugini amekutana na Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Col. Michael Mtenjele leo Julai 23, 2021 na kufanya mazungumzo kuhusu maandalizi ya safari ya wakazi wa Tarime kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango jipya la Lamai lililopo kijijini Karakatonga.

CEO Mugini ambaye pia ni Afisa Habari wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Mara, amemweleza DC Mtenjele kwamba maandalizi ya safari hiyo iliyopewa jina la “kuwapokea nyumbu Serengeti”, yamekamilika na kwamba wengi wamejitokeza kununua tiketi tayari kwa utalii wa ndani katika hifadhi hiyo ambayo ni kivutio bora barani Afrika. Mkuu huyo wa wilaya ameahidi kuungana na wakazi wa Tarime katika safari hiyo.

Safari hiyo yenye kaulimbiu inayosema “Wanyamapori Wetu, Utalii Wetu”, inahamasishwa na kuratibiwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kwa kushirikiana na Mara Online na Goldland Hotel & Tours.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages