CEO wa Mara Online, Jacob Mugini (kulia) akimuuzia mteja tiketi ya safari ya "kuwapokea nyumbu Serengeti"
IKIWA imebaki siku moja kabla ya wakazi wa wilaya ya Tarime kwenda kufanya utalii wa ndani katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kupitia lango la Lamai kijijini Karakatonga, Ofisa Mtendaji Mkuu (CEO) wa Taasisi ya Mara Online, Jacob Mugini - leo Julai 23, 2021 ameendelea kuhamasisha na kuuza kwa wananchi tiketi za safari hiyo ya “kuwapokea nyumbu Serengeti”, itakayofanyika Jumapili, Julai 25, 2021.
Safari hiyo yenye kaulimbiu inayosema “Wanyamapori Wetu, Utalii Wetu”, inahamasishwa na kuratibiwa na Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, kwa kushirikiana na Mara Online na Goldland Hotel & Tours.
Uuzaji tiketi hadi dukani
Mugini ambaye pia ni Afisa Habari wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Mara - ambayo pia inashiriki kuhamasisha safari hiyo, amesema maandalizi yamekamilika kwa asilimia 90, kwani wananchi wengi wakiwemo wafanyabiashara na kutoka taasisi mbalimbali zikiwemo za kifedha, wamejitokeza kununua tiketi za fursa hiyo ya utalii wa ndani.
CEO Mara Online, Jacob Mugini (kulia) akiuza tiketi kwa mtalii wa ndani ofisini
“Tunawapongeza wananchi waliojitokeza kununua tiketi kwa ajili ya kufanya utalii wa ndani, hili ni jambo la maendeleo katika sekta ya utalii na uhifadhi wa wanyamapori, tunamhakikishia kila mtalii wa ndani huduma bora za kitalii katika safari hiyo,” amesema Mugini.
(Habari na picha zote: Mara Online News)
No comments:
Post a Comment