NEWS

Wednesday 4 August 2021

Shirika la CDF lawanoa vijana 40 kupiga vita ndoa za utotoni Tarime
SHIRIKA la Jukwaa la Utu wa Mtoto (CDF), leo Agosti 4, 2021 limeendesha mafunzo maalumu kwa vijana 40 wa jinsia zote kutoka kata za Mwema, Regicheri, Mbogo, Binagi, Manga na Komaswa wilayani Tarime, Mara, kuhusu madhara ya ndoa za utotoni na namna ya kutokomeza tatizo hilo katika jamii.

Afisa Mawasiliano wa Shirika hilo, Celina Baragwiha (pichani juu) ameiambia Mara Online News mjini Tarime mara baada ya mafunzo hayo, kwamba wakufunzi wa mafunzo hayo, akiwemo Alice Mtuga, pia wamewapa vijana hao mbinu za kushirikiana na maofisa watendaji wa vijiji na kata. maofisa elimu na wadau wengine katika kupiga vita ndoa za utotoni.


Mkufunzi kutoka CDF, Alice Mtuga

Habari ya kina kuhusu mafunzo hayo itachapishwa kwenye toleo lijalo la gazeti la Sauti ya Mara.

MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages