NEWS

Thursday, 15 January 2026

Waziri Nyansaho azindua Bodi mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa SUMA JKT



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho (katikati waliokaa), akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa SUMA JKT aliyoizindua jijini Dodoma Januari 14, 2026.

Na Mwandishi Wetu
Dodoma
-------------

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amezindua Bodi mpya ya Ushauri ya Wakurugenzi wa Shirika la Uzalishaji Mali la Jeshi la Kujenga Taifa (SUMA JKT), itakayoongozwa na Meja Jenerali Mstaafu Michael Isamuhyo, aliyeteuliwa hivi karibuni na Waziri huyo.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dodoma jana Januari 14, 2026, Waziri Nyansaho aliwapongeza wajumbe wa Bodi hiyo kwa kuteuliwa kwao kuongoza SUMA JKT akisema shirika hilo litapiga hatua kubwa zaidi katika kukidhi madhumuni ya kuanzishwa kwake mwaka 1981.


Waziri Nyansaho akiwasilisha hotuba yake ya uzinduzi wa Bodi hiyo

Waziri Nyansaho aliwambia wajumbe hao kwamba hadi sasa shirika hilo imepiga hatua kubwa na nzuri katika miaka ya karibuni, ambapo kwa kiasi kikubwa katika uzalishaji mali na malezi ya vijana, na limekuwa na miradi mingi yenye tija kwa Taifa na kuleta maendeleo.

Aidha, Waziri Nyansaho alimpongeza Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakurugenzi wa SUMA JKT aliyemaliza muda wake, Meja Jenerali Mstaafu Farah Mohamed pamoja na bodi iliyomaliza muda wake, kwa kujituma, ubunifu na kazi nzuri iliyoleta mafanikio kwa shirika hilo.


Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho.

Waziri Nyansaho alitoa rai kwa Bodi mpya aliyoizindua kushirikiana na menejimenti katika kuyaendeleza mafanikio hayo, na pia akawataka kuongeza ubunifu ili uzalishaji na utendaji uimarike zaidi.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages