NEWS

Friday 6 August 2021

Tarime wazindua chanjo ya UVIKO -19, DC aonya upotoshaji

 

MKUU wa Wilaya ya Tarime (DC) Col. Michael Mntenjele amezindua rasmi zoezi la kutoa chanjo dhidi ya UVIKO-19 (Corona) na kuwataka wananchi walio katika makundi yanayolengwa kujitokeza  kupata chanjo hiyo.

DC  Mntenjele  pamoja na Katibu Tawala (DAS) wa wilaya hiyo John Marwa na wajumbe wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya wamechanjwa wakati wa uzinduzi wa zoezi hilo ambalo limefanyika mapema leo Agositi 6,2021 katika hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Tarime

DC Tarime akipata chanjo dhidi ya UVIKO-19

 Aidha mkuu huyo wa wilaya amekemea watu wanatoa tarifa za upotoshaji  kuhusiana na chanjo hiyo  na kuwataka wananchi kuwapuuza.

Amesema pia suala kuchukua tahadhari  dhidi ya maambukizi ya virus vya Corona lazima yaendelee kuzingatiwa hata kwa wale ambao watachanjwa.

“Pamoja na kuwa tutakuwa tumepata chanjo hatua zingine za kujikinga na kuwakinga wengine ziendelee kuchukuliwa”, amesisitiza DC Mntenjele.

DC Mntenjele akiongea na wananchi waliojitokeza kupata chanjo leo Ijumaa

Aidha katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mara Ally Hapi jana alizindua zoezi la kutoa chanjo  dhidi ya UVIKO-19 kimkoa  mjini Musoma jana.

DAS Marwa akipata chanjo ya UVIKO-19
 (Habari, picha na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages