NEWS

Tuesday 28 September 2021

Wananchi wamiminika kumjulia hali, kumpa pole Mbunge Ghati




WANANCHI wameendelea kumiminika nyumbani kwa Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Mara, Ghati Zephania Chomete, kumjulia hali na kumpa pole kutokana na ajali aliyopata.

Mbunge Ghati na mume wake, Marwa Mathayo walipata ajali ya gari mkoani Tabora, miezi michache iliyopita.

Jana Jumatatu kundi jingine la wananchi, wakiwemo viongozi wa jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Jimbo la Musoma Mjini, wamefika nyumbani kwake mjini Musoma kumjulia hali na kumpa pole.

Mbunge Ghati (kulia) na mume wake, Marwa (kushoto waliokaa), wakiwa katika picha ya pamoja na wananchi waliokwenda kuwajulia hali nyumbani kwao.

Katibu wa UWT Mkoa wa Mara, Sarah Kairanya, amewapongeza viongozi hao kwa kuona umuhimu wa kumjulia hali Mbunge Ghati na kumpelekea misaada mbalimbali.

Kairanya amewataka wananchi kuendelea kumwombea baraka za Mungu afya yake izidi kuimarika, ili arejee kuendelea na majukumu ya kutumikia umma.



Mbunge Ghati amewashukuru viongozi hao na makundi mengine ya wananchi ambayo yameendelea kujitokeza kumjulia hali, kumpa pole na misaada ya hali na mali.

(Imeandikwa na Maximillian Ngessi, Musoma)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages