NEWS

Friday 10 September 2021

Watalii wa ndani kuzuru Makumbusho ya Baba wa Taifa Butiama keshoAfisa Habari wa TPO Mkoa wa Mara, Jacob Mugini.

KUNDI la watalii wa ndani 20, wengi wao wakiwa viongozi na wanachama wa Taasisi ya Kizalendo Tanzania (TPO) Mkoa wa Mara, kesho Septemba 11, 2021 wanatarajia kutembelea Makumbusho ya Mwalimu Julius K. Nyerere yaliyopo Butiama.

“Kundi hili la watalii wa ndani pia litatembelea makazi ya Baba wa Taifa na baada ya chakula cha mchana, litatembelea hoteli za kitalii zilizopo kandokando ya Ziwa Victoria, ikwemo Matvilla Beach,” Afisa Habari wa TPO Mkoa wa Mara, Jacob Mugini ameiambia Mara Online News leo jioni.
Sehemu ya Hoteli ya Matvilla Beach

Mugini amesema safari hiyo imeandaliwa na uongozi wa TPO Mkoa wa Mara na Kampuni ya Mara Online Safaris.

“Maandalizi yote yamekamilika na tunategemea wageni wata- enjoy,” Mugini ambaye pia ni Mkurugenzi wa Mara Online Safaris amethibitisha.

Kampeni ya utalii wa ndani nchini inaendelea kuhamasishwa na vyombo vya habari vya Mara Online, yaani Blogu ya Mara Online News na Gazeti la Sauti ya Mara, huku Kampuni za Mara Online Safaris na Goldland Hotel & Tours zikishirikiana kuratibu safari za kutembelea vivutio vya utalii.

Kampeni hizo na vyombo hivyo vya habari vimeonesha mafanikio makubwa, baada ya watalii wa ndani zaidi 100 kuhamasika na kujitokeza kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Serengeti, hivi karibuni na sasa Makumbusho ya Baba wa Taifa Butiama.


Baadhi ya viongozi na wanachama wa TPO katika picha ya pamoja na wahifadhi ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.

Wanachama na viongogi wa TPO ni miongoi mwa watalii wa ndani waliotembelea hifadhi hiyo katika safari ya hivi karibuni, iliopewa jina la Twenzetu Kuwapokea Nyumbu Serengeti.

Safari hiyo ilihusisha watalii wa ndani zaidi ya 60, akiwemo Mkuu wa Wilaya (DC) ya Tarime, Col. Michael Mntenjele, ambapo walishuhudia vivutio mbalimbali, ikiwemo misafara ya makundi ya nyumbu na idadi kubwa ya viboko wakivinjari katika mto Mara.
Nyumbu wakifurahia mazingira Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti

DC Mntenjele (wa pili kushoto), Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Tarime, Daudi Ngicho (kushoto), Mkurugenzi wa Mara Online Safaris, Jacob Mugini (kulia) na watalii wengine wa ndani walipokwenda kujionea viboko wakivinjari katika Mto Mara ndani ya hifadhi hiyo.

(Habari na picha zote: Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages