NEWS

Tuesday 18 January 2022

Profesa Muhongo achanga Sh milioni 3 za maji ya kunywa sherehe za CCM TaifaMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo ametoa mchango wa shilingi milioni 3 za kununua maji ya kunywa - yatakayotumika wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM), yatakayofanyika kitaifa Februari 5, 2022 mkoani Mara.

Profesa Muhongo ametoa mchango huo leo Januari 18, 2022, kupitia benki ya CRDB Musoma kwenda akaunti ya kiwanda cha maji cha Ochele.

Baadaye mbunge huyo amekwenda kukabidhi risiti ya mwamala wa mchango huo kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Mara, Langaeli Akyoo).

Profesa Muhongo (kushoto) akimkabidhi Akyoo risiti ya CRDB ya kuweka mchango huo wa shilingi milioni 3, katika ofisi za CCM Mkoa wa Mara, mjini Musoma.

Kwa mujibu wa Akyoo, maadhimisho hayo ya CCM yatafanyika kwenye viwanja vya Mkendo mjini Musoma, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages