NEWS

Tuesday 1 February 2022

RC awahakikishia waandishi wa habari usalama ziara ya Rais Samia mkoani MaraMKUU wa Mkoa (RC) wa Mara, Ally Hapi, amewahakikishia waandishi wa habari usalama wakati wa ziara ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan.

Rais Samia anatarajiwa kufanya ziara ya siku nne (Februari 4 – 7, 2022) mkoani Mara, ambapo atapata fursa ya kushiriki maadhimisho ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa CCM, kukagua na kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.

Akizungumza na waandishi wa habari wa mkoani Mara mjini Musoma jana, RC Hapi amesema ofisi yake imejipanga kuhakikisha wanashiriki ziara ya Rais katika mazingira salama na bila vikwazo.RC Hapi akizungumza katika mkutano huo

 RC Hapi amesisitiza kuwa waandishi wa habari ni kundi muhimu na lina haki ya kupata habari za ziara ya Rais Samia kwa ajili ya kuhabarisha umma, hivyo usalama wao lazima uzingatiwe. “Tungependa muwe salama ndugu zangu,” amesisitiza.

Pamoja na mambo mengine, mkuu huyo wa mkoa ameelekeza Afisa Habari wa Mkoa wa Mara kuandaa vitambulisho maalumu vitakavyowezesha waandishi wa habari kushiriki ziara ya Rais Samia bila kikwazo.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages