NEWS

Tuesday 29 March 2022

Mamilioni kugharimia usambazaji maji Musoma Vijijini, wananchi wamshukuru Rais SamiaSERIKALI imetoa shilingi milioni 600 chini ya mpango wa kupambana na UVIKO-19, kwa ajili ya kugharimia usambazaji wa maji ya bomba kwenye baadhi ya vijiji katika halmashauri za wilaya ya Musoma na Butiama mkoani Mara.

Usambazaji wa huduma hiyo ya maji utatekelezwa kupitia mradi wa bomba la maji wa Mugango - Kiabakari - Butiama.

Kiasi hicho cha fedha kimegawanywa sawa, yaani shilingi milioni 300 kwa kila halmashauri.

“Kwa upande wa halmashauri yetu [Halmashauri ya Wilaya ya Musoma], fedha hizo [shilingi milioni 300] zitatumika kusambaza maji ya bomba kutoka Mugango kwenda vijiji vya Nyasaungu (Kata ya Ifulifu) na Kurwaki (Kata ya Mugango),” imeeleza sehemu ya taarifa kwa vyombo vya habari, iliyotolewa na ofisi ya Mbunge Jimbo la Musoma Vijijini, leo.

Wakazi, viongozi wa kata na vijiji vilivyolengwa na mradi huo na Mbunge wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo (pichani juu), wameishukuru Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan, kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuwatatulia kero ya ukosefu wa maji ya bomba.

(Imendikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages