NEWS

Thursday 31 March 2022

Meneja Shirika la Bima la Taifa Mkoa wa Mara atembelea ofisi za Mara Online



MENEJA wa Shirika la Bima la Taifa (NIC) Mkoa wa Mara, Aurelia Joseph, leo ametembelea ofisi za chombo cha habari cha kidijitali cha Mara Online News na gazeti la Sauti ya Mara, na kutumia fursa hiyo kutoa wito kwa wananchi wa mkoa huo kutumia huduma za bima za shirika hilo - ambazo amesema zimeendelea kuboreshwa zaidi kukidhi matarajio ya wateja.


Meneja wa NIC Mara, Aurelia (kulia) na CEO wa Mara Online, Jacob Mugini wakiendelea na mazungumzo ofisini.

Vyombo vya habari vya Mara Online na gazeti la Sauti ya Mara vimeendelea kuvutia wasomaji na wadau kila kona ya mkoa wa Mara na maeneo mengine nchini na nje ya Tanzania.

Vyombo hivyo vimejikita zaidi katika kuripoti habari za maendeleo ya jamii, uchumi, uhifadhi wa vyanzo vya maji, mazingira na wanyamapori.

“Umakini na ubora wa habari zetu ambazo zinasaidia kuhamasisha maendeleo na uhifadhi wa mazingira na wanyamapori, ni baadhi ya vitu vinavyotufanya kuwa tofauti na vyombo vingine,” amesema Jacob ambaye kitaaluma ni mwandishi wa habari, akibobea kwenye uandishi wa habari na makala katika lugha za Kiswahili na Kiingereza.

CEO Mara Online, Jacob Mugini

#MaraOnlineNews-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages