NEWS

Friday 22 April 2022

Rais mstaafu wa Kenya Mwai Kibaki afariki dunia, Rais Uhuru atangaza maombolezoRAIS wa zamani wa Kenya, Mwai Kibaki (pichani), amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 90.

Rais Uhuru Kenyatta ametangaza kifo cha Kibaki muda mfupi uliopita kupitia runinga mbalimbali nchini Kenya.

Kibaki alikuwa Rais wa tatu wa Jamhuri ya Kenya kutoka mwaka 2002 hadi 2013.


Mwai Kibaki akikagua Gwaride la Heshima la Jeshi wakati akiwa Rais wa Jamhuri ya Kenya

Rais Uhuru amesema kiongozi huyo wa zamani wa Kenya aliaga dunia jana Alhamisi na kwamba ataandaliwa mazishi ya kitaifa.

Anamuomboleza mtangulizi wake huyo kama kiongozi aliyeleta ukuaji wa uchumi, demokrasia na kuimarisha hali ya uchumi ya Wakenya.

Aidha, Rais Uhuru anamkumbuka Kibaki kwa juhudi zake zilizowezesha kupatikana kwa Katiba mpya ya mwaka 2010 na kuongoza uidhinishaji wake.

Amesema bendera zote katika majengo ya umma, wizara na balozi zote duniani zitapepea nusu mlingoti hadi pale mwili wa Kibaki utakapozikwa. BBC

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages