NEWS

Tuesday 31 May 2022

TAKUKURU yawafikisha mahakamani mabosi wa Mamlaka ya Maji Bunda kwa ubadhirifuTAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) Wilaya ya Bunda mkoani Mara, imewafikisha mahakamani viongozi wawili wa Mamlaka ya Maji Bunda kwa mashtaka matatu tofauti.

Viongozi hao, Afisa Utumishi, Mujo Bulongo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka hiyo, Marichela Maisha, walifikishwa na kusomewa mashtaka hayo katika Mahakama ya Wilaya ya Bunda, jana.

Wanashtakiwa kwa matumizi mabaya ya madaraka, kutumia nyaraka kwa lengo la kumdanganya mwajiri na ubadhirifu wa mali ya umma.

Mtuhumiwa wa kwanza, Bulongo, anadaiwa kuandaa dokezo na mtuhumiwa wa pili, Maisha, kuidhinisha kwenye dokezo hilo yafanyike malipo ya shilingi milioni 1.3 kwa watumishi - kama malipo ya kazi tofauti za ziada, huku muda na tarehe za kazi hizo vikifanana na malipo kutolewa mara mbili kwa tarehe, saa na watu walewale.

Kesi hiyo imesajiliwa mahakamani hapo kama Economic Case No. 06/2022, mbele ya Hakimu Sokanya.

Watuhumiwa wote amekidhi masharti ya dhamana na kesi hiyo imepangwa Juni 28, mwaka huu kwa ajili ya kuwasomea hoja za awali.

(Imeandikwa na Mara Online News)

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages