NEWS

Wednesday 20 July 2022

Rais Samia amteua Camillus Wambura kuwa IGP, Sirro Balozi Zimbabwe


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amempandisha cheo na kumteua Kamishna wa Polisi Camillus Mongoso Wambura (pichani juu) kuwa Inspekta Jenerali na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Tanzania.

Kabla ya uteuzi huo, Kamishna Wambura alikuwa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) nchini.

Kulingana na taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Juhura Yunus leo, Rais Samia amemteua aliyekuwa IGP, Simon Nyakoro Sirro kuwa Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe.

#SautiYaMaraDigital-Updates

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages